Februali 2016, Mkuu wa Mkoa wa Jiji la Dar es salaam Paul Makonda aliweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa Hospital ya Mama na Mtoto Eneo la Chanika, Ilala jijini humo chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Korea Kusini (KOICA).
Baada ya Miezi kadhaa ya Ujenzi huo, Leo Mkuu Mkoa wa Jiji hilo Paul Makonda, akiongozana na Mkuu wa Wilaya wa Ilala Sophia Mjema wamefanya ukaguzi katika Hospital hiyo ambapo amesema ujenzi huo utakamilika mwezi juni na kwamba kukamilika kwake kutasaidia jitahada za kupunguza vifo vya Mama na mtoto wakati wa kujifungua.
Mganga mkuu wa Mkoa huo Grace Maghembe amesema vifaa na mfumo mzima wa hospitali hiyo umefungwa katika teknolojia ya Kisasa na kwamba nakuifanya kuwa Hospitali pekee katika jiji hilo itakayo kuwa na huduma za kisasa zaidi na kupunguza misongamano katika Hospitali za Muhimbili, Amana na Mnazi Mmoja.
Mara baada ya kukamilika kwa ujenzi huo baadhi ya huduma zitakazotolewa ni pamoja na X-Ray, Upasuaji mkubwa na mdogo, Kujifungua, Watoto njiti.
Kamujibu wa RC Makonda Hospitali hiyo itazinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli
No comments
Post a Comment