Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Monday, February 27, 2017

KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI CHAPOKEA MSAADA WA VIFAA VYA KUZUIA VUMBI KWA ASKARI


1
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, akipokea vifaa vya kuzuia vumbi kwa askari wa usalama barabarani  kutoka kwa msamaria mwema, Tahir Othman (kulia) ,aliyejitolea vifaa hivyo ili kusaidia askari  kuepukana na vumbi kuingia kwenye njia ya hewa  wawapo katika shughuli zao.Anayeshuhudia katikati ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni .Makabidhiano hayo yamefanyika ofisini kwa Naibu Waziri,jijini Dar es Salaam.
2
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, akionyesha kwa waandishi wa habari  jinsi ya kuvaa kifaa cha  kuzuia vumbi kwa askari wa usalama barabarani  alivyopokea kutoka kwa msamaria mwema,Tahir Othman(hayupo pichani) ,aliyejitolea vifaa hivyo ili kusaidia askari  kuepukana na  vumbi kuingia kwenye njia ya hewa wawapo katika shughuli zao.Kushoto ni  Naibu Waziri wa Wizara ya  Mambo ya Ndani ya Nchi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni. Makabidhiano hayo yamefanyika ofisini kwa Naibu Waziri, jijini Dar es Salaam.
3
Naibu Waziri wa Wizara  ya Mambo ya  Ndani ya Nchi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama  Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni, akiangalia jinsi ya kuvaa kifaa cha kuzuia vumbi kwa askari  kutoka kwa  Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, ambae pia ni Katibu Mtendaji wa baraza hilo.Vifaa hivyo vilitolewa na msamaria mwema,Tahir Othman (hayupo pichani).Makabidhiano hayo yamefanyika ofisini kwa Naibu Waziri,jijini Dar es Salaam.
Chanzo:
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment