Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Monday, February 27, 2017

Chimeledya: Waumini msichanganywe na maneno


Askofu Mkuu wa Anglikana Tanzania, Dk Jacob Chimeledya amesisitiza kuwa dayosisi ya Dar es Salaam ipo chini yake katika kipindi hiki baada ya Askofu Dk Valentino Mokiwa kuamriwa kujiuzulu.

Aliwataka waumini wasichanganywe na maneno  kwani taratibu na katiba ilifuatwa katika kumuondoa Mokiwa.

"Nawaomba waumini wa kanisa hili kuwa  watulivu, msichanganye na maneno yanayosemwa juu ya uamuzi wa kumtaka Dk Mokiwa kujiuzulu.Tulifuata taratibu zote na hivi sasa mimi ndiye msimamizi mkuu wa dayosisi hadi hapo askofu wa jimbo atakapopatikana," amesema Dk Chimeledya

Dk Chimeledya ametoa msisitizo huo leo wakati aliposhiriki ibada ya misa ya asubuhi  iliyoongozwa na Jaji mstaafu Augustino Ramadhan iliyofanyika katika kanisa la St Albano Posta na kusema kuwa Katiba inaruhusu yeye kulisimamia kanisa kutokana na Mokiwa, kutakiwa kujiuzulu .

Amesema mchakato wa kumuamuru Dk Mokiwa aliyekuwa  askofu mkuu wa dayosisi hiyo ulifuata sheria , kanuni na katiba ya Anglikana iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2004.
Chanzo: Muungwana Blog
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment