Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Sunday, August 10, 2014

Machumu mshindi tuzo uongozi Afrika Mashariki


 
Na Ndaya Mgoyo, MwananchiNairobi. Kampuni inayofanya utafiti wa Utawala Bora katika nchi za Afrika ya CEO Titans Building Nations ya Afrika Kusini, imemtunuku tuzo mbili Mhariri Mtendaji Mkuu wa Mwananchi Communications Limited (MCL), Bakari Machumu.
Kampuni ya Mwananchi ndiyo inayochapisha magazeti ya Mwananchi, Mwanaspoti na The Citizens.
Machumu alipata Tuzo ya Uongozi Thabiti katika Vyombo vya Habari vya Tanzania, pia Afrika Mashariki.
Upande mwingine, Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi nchini, Titus Kamani naye alikabidhiwa Tuzo ya Utawala Bora katika kipengele cha Watendakazi Bora wa Serikalini wa Afrika.
Machumu na Waziri Kamani walikabidhiwa tuzo hizo juzi usiku katika hafla iliyofanyika Hoteli ya Hilton jijini Nairobi, Kenya.
Kampuni CEO Titans Building Nations inajihusisha na kutambua watu wanaofanya kazi kwa juhudi kwa ajili ya maendeleo ya mataifa yao, hata kuthubutu kuvuka mipaka katika utekelezaji wa majukumu yao.
Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo, Machumu alisema kuwa amefurahi na ni fahari kubwa kuona kazi yake na taaluma ya habari kwa jumla vikithaminiwa.
“Vyombo vya habari vina jukumu la kuleta mabadiliko katika jamii. Viongozi wa nchi za Afrika wanatakiwa kufahamu mchango wa vyombo vya habari na kushirikiana navyo katika kufikisha habari kwa jamii,” alisema na kuongeza:
“Viongozi wa nchi za Afrika na Tanzania kwa jumla, wanatakiwa kuruhusu watu kuzungumza mambo kwa uwazi na wasifanye vyombo vya habari kuwa ni maadui, bali washirikiane navyo katika kuleta maendeleo.”
Naye Waziri Dk Kamani alisema amefurahia tuzo hiyo na kwamba inaonyesha jinsi wizara yake inavyofanya kazi kwa usahihi na kutambulika hata nje ya mipaka ya Tanzania.
“Nimeshangaa kuona kazi ya wizara yangu imetambuliwa namna hii. Tuzo hii si yangu pekee, bali ni ya wafanyakazi wote wa wizara, pia Watanzania kwa jumla,” alisema.
Waziri huyo alitoa wito kwa viongozi wa Afrika wajitahidi kuwatumikia watu wote ili kusukuma mbele maendeleo.
Katika tuzo hizo mshindi wa jumla alikuwa Dk Manilal Chandaria wa Kenya, ambaye ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Comcraft Group. Alitunukiwa tuzo ya nchini kwake na Afrika.
Katika kipengele cha Utawala Bora wa Taasisi za Kijamii, Dk Abbas Gullet wa Kenya Red Cross, alipata tuzo ya nchini kwake wakati Evans Wadongo wa Kenya alipata Tuzo ya Afrika Mashariki.
Washindi wengine ni Amos Wakes wa Uganda (Utalii), Benson Kairuki Kitabu wa Kenya (Fedha), Mekonnen Tesfaye wa Ethiopia (Mawasiliano).
Awali Mkurugenzi wa CEO Titans Building Nations, Annelize Wapener alisema kuwa karne ya 21 ni kwa ajili ya maendeleo na uthabiti wa Afrika na kwamba kampuni yake inataka kuona nchi za Afrika zinaungana katika kutoa mafanikio bila kujali mipaka iliyopo.
Jumla ya washiriki 100 walichaguliwa kutoka taasisi mbalimbali Afrika na wawakilishi 28 kutoka katika nchi 19 za Afrika waliingia kwenye fainali.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment