Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Sunday, August 10, 2014

Obama: Marekani haitobururwa katika vita vingine Irak

Moshi ukionekana hewani baada ya shambulizi la Marekani dhidi ya vituo vya wanamgambo wa Isamic State karibu na Khazer kaskazini mwa Irak
Moshi ukionekana hewani baada ya shambulizi la Marekani dhidi ya vituo vya wanamgambo wa Isamic State karibu na Khazer kaskazini mwa Irak
Rais Barack Obama amesema hatoruhusu kundi la wanamgambo wa kislamu huko Irak kuunda taifa la kando Irak ili kuweza kuwa na hifadhi ya salama kwa ajili ya  ugaidi.
Akizungumza na waandishi habari Jumamosi, kiongozi huyo wa Marekani amesema "sidhani tutaweza kutanzua mzozo huo mnamo muda wa wiki chache, itabidi wa Irak wenyewe watafute suluhisho kwa mzozo wao, wakiwa na utawala wa umoja wa Irak."
Wanajeshi wa marekani watayarisha chakula cha kudondoshwa IrakWanajeshi wa marekani watayarisha chakula cha kudondoshwa Irak
Ndege za kijeshi za Marekani zilifanya mashambulizi mawili dhidi ya vituo vya kundi la Islamic State huko kaskazini magharibi ya Irak, siku ya Ijuma na kuharibu silaha na vifaa vyao.
Wakati huo huo ndege za kijeshi zimedondosha chakula nja mahitaji ya dharura siku ya Jumamosi kwenye mlima Sinjar, ambako maelfu ya wa Iraki wamekimbilia kufuatia mashambulizi ya wanamgambo wa Islamic State.
Rais Obama amesema aliamua kuchukua hatua hizo huko Irak kwa sababu Marekani haiwezi kukaa kimya wakati raia wasio na hatia wanakabiliwa na mauwaji, lakini haitioruhusu marekani kubururwa tena katika vita vya nchi kavu nchini humo.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment