Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, March 19, 2014

UTAFITI: KANISA LA SABATO LINA WANAWAKE WENGI KULIKO WANAUME


Baadhi ya waimbaji wa kwaya maarufu nchini ya kanisa la sabato Kurasini, wakiwa katika moja ya huduma.
Tafiti zimeonyesha kuwa kanisa la Waadventista Wasabato linaidadi kubwa ya washiriki ya wanawakike ikilinganishwa na wakiume.

Hayo yameelezwa na mmoja wa makamu wa Rais wa Kanisa la Waadventista Wasabato ulimwenguni Daktari Mchungaji Benjamini Schoun katika ukumbi wa Advent Hill uliopo makao makuu ya kanisa la Waadventista Wasabato ya Afrika Mashariki na Kati jijini Nairobi katika warsha ya teknolojia ya habari na mawasiliano

Daktari Schoun ameongeza kuwa,mbali na idadi ya wanawakike kuwa kubwa,idara ya shule ya sabato imeendelea kufanya vizuri sana ikilinganishwa na idara mbalimbali za kanisa.Hata hivyo imeonekana ni idadi ndogo ya washiriki wanao wapeleka watoto wao kupata elimu katika shule za kanisa.

Warsha ya teknolojia ya habari na mawasiliano imemalizika jana iliwakutanisha wajumbe kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika na Ulaya, hata huku wajumbe wakionyesha kufurahishwa na wakufunzi mbalimbali walio simama katika zamu zao.

Na. Miller James-Nairobi/Networkedblogs
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment