Writen by
sadataley
5:10 PM
-
0
Comments
Bango kubwa la kanisa la Atlah World Missionary lililopo maeneo ya Harlem jijini New York nchini Marekani lisemalo "Yesu angewapiga mawe watu wanaojihusisha mapenzi ya jinsia moja" limezua maswali kwa wanaharakati wanaopigania haki za watu wanaofanya mapenzi ya jinsia moja LGBT nchini Marekani.
Kwa mujibu wa mchungaji wa kanisa hilo James David Manning ameuambia mtandao wa Christian Postkwamba bango hilo wameliweka wiki moja iliyopita ikiwa ni kusema ukweli tofauti na wanaharakati hao wa LGBT ambao wamekuwa wakizungumza maswala ya Yesu na Biblia."Wamekuwa wakisambaza uongo kuhusu Yesu angefanyaje juu ya watu wanaojihusisha na vitendo vya mapenzi ya jinsia moja, kama ni kweli Yesu amewahi kuzungumzia suala hilo ama na Biblia inasemaje kwa upana wake kuhusu vitendo hivyo, kwahiyo tumeamua kusema nini Yesu angefanya kwa watu hao", amesema mchungaji Manning.
Mchungaji Manning pia amesema wanafikiria kuliacha bango hilo eneo hilo mpaka hapo watakapoona ujumbe umewafikia walengwa na kuleta maana ya Kristo. Ujumbe huo umeibua maneno kutoka kwa wanaharakati mbalimbali wa jamii hiyo kupitia tovuti zao. Kwa mujibu wa blogger aitwaye Jervis aliandika kwamba mwezi uliopita mchungaji Manning aliweka bango kubwa likisema Rais Barack Obama amewarushia mapepo ya kishoga wanaume weusi, na leo tena ameonyesha upendo wa Kristo kwa kuweka bango hilo.
Ujumbe uliowekwa na kanisa hilo umepokelewa kitofauti na watu mbalimbali walioweka meseji zao kwenye mtandao wa Facebook wa tovuti ya Christian Post wengi wakienda kinyume na mchungaji huyo wakisema si kweli kwamba Yesu angewapiga mawe bali angewaleta kanisani wahubiriwe habari njema na kuachana na uasi wao.
No comments
Post a Comment