Writen by 
                            sadataley
3:53 PM
                            - 
                            
0
                            Comments
                          
Wajumbe Bunge la Katiba,  wakifuatilia mada mbalimbali za  Kanuni za Bunge hilo mjini Dodoma wakati wa semina ya kupitia kanuni hizo. Picha na Michael Jamson 
Na Sharon Sauwa, Mwananchi
Dodoma. Wajumbe wa Bunge la Katiba wameelezwa kuwa ndani Bunge hilo hakuna Waziri Mkuu, Makamu wa Rais wala mawaziri, wote wana hadhi sawa.
Hayo yalisemwa bungeni na Mjumbe wa Kamati ya Kanuni ya Bunge hilo, Ussi Jecha Sima,  alipokuwa akijibu maswali ya wajumbe.
“Kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na Kanuni tulizozitunga humu ndani, hamna mawaziri, wote hapa ni wajumbe wote tuna hadhi na status (nafasi) sawa,” alisema.
Awali akichangia semina hiyo ya kanuni, Luis Majaliwa alisema, juzi wakati Mwenyekiti wa Bunge, Samuel Sitta, alipokuwa akiahirisha Bunge alimwomba Mwanasheria Mkuu wa Serikali kutoa hoja ambayo iliungwa mkono na mawaziri walioko katika Bunge hilo.
“Kwa sababu katika Bunge la Jamhuri wanaopaswa kuunga mkono hoja ni mawaziri, je,katika Bunge hili ambapo tupo mawaziri wa Bunge la Muungano, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kundi la 201 ni utaratibu gani unaopaswa kutumika?” alihoji.
 
 
 
 
 
 
 
No comments
Post a Comment