Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Saturday, March 22, 2014

AMISOM wameuteka mji Koryoley, Somalia

Al Shabaab
Wanajeshi wa Muungano wa Afrika wanameuteka mji muhimu wa Koryoley, ulio umbali wa kilomita 90 Kusini Magharibi mwa mji mkuu Mogadishu.
Mji wa Koryoley, umekuwa chini ya udhibiti wa kundi la wanamgambo la Al Shabaab kwa miaka mitano iliyopita.
Kutekwa kwa mji huo ni ukombozi tangu kuanza harakati hizo dhidi ya Al Shabaab mwezi Machi mwaka jana wakiungwa mkono na Umoja wa Mataifa.Mwandishi wa BBC aliye katika eneo hilo anasema kulikuwa mlio wa silaha na baadhi ya raia wa mji wamekimbia.
Wanajeshi hao wamefanikiwa kukomboa miji mingine muhimu na hata kuwatimua wapiganaji hao kutoka katika ngome zao kubwa.

Wengi wa wanajeshi wa AU ni kutoka Uganda, wakisaidiwa na wanajeshi wa Kenya, Burundi na sasa Ethiopia pamoja na wanajeshi wa Somalia.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment