Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Saturday, November 9, 2013

Nigeria watwaa ubingwa wa dunia wa FIFA 2013 wachezaji walio chini ya umri wa miaka 17

Wachezaji wa Nigeria wakishangilia ushindi, 10 November 2013

Na Flora Martin Mwano
Timu ya soka ya Nigeria imenyakua kombe la dunia la michuano ya soka kwa wachezaji walio na umri wa chini ya miaka 17 (U-17) iliyopigwa katika dimba la Mohammad Bin Zayeb huko falme za kiarabu. Vijana hao wameandika historia ya pekee baada ya kupachika mabao 3-0 dhidi ya Mexico katika fainali za siku ya ijumaa.

Bao la kwanza lilipachikwa katika dakika ya 9 ambapo Mexico ilijifunga yenyewe kupitia kwa mchezaji wake Eric Aguirre.
Katika nusu ya pili ya mchezo huo Nigeria iliongeza mabao mawili kupitia Kelechi Iheanacho na Musa Mohammed.
Nigeria ilitwaa kombe hilo katika miaka ya 1985, 1993, 2007 na ushindi wa sasa unaipa historia ya pekee ya kuwa Taifa pekee duniani lililotwaa ubingwa huo kwa mara nne.
Rais wa Shirikisho la soka duniani FIFA, Sepp Bletter ni miongoni mwa vigogo wa soka waliofika Abu Dhabi kushuhudia mtanange huo.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment