Latest News

GNM Cargo

GNM Cargo
GNM CARGO & LOGISTICS

menu

Tuesday, June 6, 2017

Singida United yapigwa 5 - 4, yafungasha virago

Dar es Salaam. AFC Leopards imekuwa timu ya kwanza kufuzu kwa robo fainali ya mashindano ya SportPesa kwa kuifunga Singida United  penalti 5-4. baada ya kumaliza dakika 90 kwa sare 1-1 kwenye Uwanja wa Uhuru.

Katika mchezo huo Singida United ilikuwa ya kwanza kupata bao lililofungwa dakika ya 10 na Kutinyu  Tafadzwa, kabla ya miamba ya Kenya, AFC Leopards kusawazisha katika dakika ya 63, kupitia kwa Vicent Oburu.

Waliofunga penalti kwa Singida United ni Atupele Green,  Shango Hamis,  Nhivi Simbarashe na Muroiwa Elisha wakati Chuku Salum akipaisha.

Waliofunga penalti kwai AFC ni Bernard Mangoli,  Marselas Ingotsi,  Kateregga Allan,  Duncan Otieno na Fiamenyo Gilbert.

Kocha wa Singida United, Hans Pluim ameanza vibaya kibarua chake baada ya kutupwa nje mashindano ya Sport Pesa.

Huu nii mchezo wa kwanza kwa Pluijm tangu alipoanza kuinoa timu hiyo iliyopanda daraja.

Wakati huohuo;  mashabiki wa Simba wameahidi kula sahani moja na Singida United baada ya kubaini timu hiyo ina mahaba na Yanga.

"Hawafiki mbali, tumeshabaini wamekuja Ligi Kuu kwa kazi gani. Na watambue Simba iko kamili,"alisema Said  Salum shabiki wa Simba
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment