Latest News

GNM Cargo

GNM Cargo
GNM CARGO & LOGISTICS

menu

Tuesday, June 6, 2017

Mzozo wa safari za anga wakolea Qatar

qatar

Image captionshirika la anga la Qatar
Mgawanyiko kati ya nchi ya Qatar na nchi kadhaa za jirani kuongezeka kwa hali ya kukatizwa kwa safari za anga.
Saudi Arabia, Bahrain na Misri wamethibitisha kwamba nao watasitisha safari za anga kuelekea Qatar kuanzia leo.Mashirika makubwa ya anga ya kikanda, ikiwemo Emirates na Etihad, ni miongoni mwa mashirika yatakayo sitisha safari za anga nchini humo.
Qatar imekanusha madai kwamba inasaidia watu wenye msimamo mkali na kuyaita madai hayo kama upotoshaji kamili.
Serikali ya nchi hiyo imesema kwamba mzozo huo hautaathiri chochote katika utaratibu wa maisha , ingawa kuna taarifa za wananchi kuanza kuhifadhi chakula kama dharula tangu mzozo huo ulipoibuka siku ya Jumatatu wiki hii.
Nchi ya Saudi Arabia tayari imekwisha tangaza kufungwa kwa mpaka pekee wa aridhini na Qata.
BBC
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment