Latest News

GNM Cargo

GNM Cargo
GNM CARGO & LOGISTICS

menu

Tuesday, June 6, 2017

Korea Kaskazini: Marekani ndiyo iliyounda makundi ya kigaidi Mashariki ya Kati

Balozi wa Korea Kaskazini anayehusika na masuala ya nchi za Kiarabu za eneo la Ghuba ya Uajemi amekosoa vikali siasa za uhasama za serikali ya Marekani katika eneo la Mashariki ya Kati na kubainisha kuwa, Washington ndiyo inayohusika na uundwaji wa makundi yote ya kigaidi katika eneo.
So Chang Sik ameyasema hayo katika mazungumzo na gazeti la al-Rai la nchini Kuwait ambapo sambamba na kuashiria juu ya harakati za makundi ya kigaidi katika eneo la Mashariki ya Kati amesema kuwa, muhusika mkuu wa kuundwa magenge yote ya kigaidi likiwemo kundi la al-Qaidah na Daesh (ISIS) ni Marekani. 
So Chang Sik ameongeza kuwa, Washington inatekeleza siasa zake za kuibua tofauti na mifarakato katika maeneo tofauti ya dunia. Kadhalika balozi huyo wa Korea Kaskazini amezungumzia siasa za Marekani za kuingilia mambo ya ndani katika eneo la Peninsula ya Korea na kuongeza kuwa, Washington inaendesha vitisho dhidi ya Pyongyang na kusisitiza kuwa, Korea Kaskazini imejiandaa kujibu vitisho vyote vya Marekani kwa nguvu zake zote. Amesema  iwapo Marekani itakiuka haki ya kujitawala ya Korea Kaskazini basi Pyongyang itazisambaratisha kambi za kijeshi za nchi hiyo katika eneo.
Mwanadiplomasia huyo wa Korea Kaskazini amesema kuwa, Pyongyang inaunga mkono juhudi zozote zenye lengo la kudumisha usalama na amani katika eneo la Korea, lakini kwamba haipo tayari kufanya muamala unaokiuka haki yake ya kujitawala.
Parstoday
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment