Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, November 2, 2016

Shirika lapendekeza Yahya Jammeh awekewe vikwazo.

Yahya Jammeh

Image copyrightAFP
Image captionYahya Jammeh aliingia madarakani mwaka 1994 kupitia mapinduzi
Shirika la kimataifa la kutetea haki za kibinadamu la Human Rights Watch alimetoa wito kwa jamii ya kimataifa kumshinikiza zaidi Rais wa Gambia Yahya Jammeh.
Shirika hilo linasema kiongozi huyo amekuwa akiwahangaisha wapinzani wake uchaguzi mkuu wa mwezi ujao unapokaribia.
Kwenye ripoti mpya, shirika hilo linasema wanaharakati wawili wamefariki wakiwa kizuizini na wengine kadha wanazuiliwa gerezani, bila huduma za kimatibabu na mawakili.
HRW wametoa wito kwa majirani wa Gambia pamoja na Umoja wa Ulaya na Marekani kuingilia kari.
Shirika hilo linataka kiongozi huyo pamoja na washirika wake wawekeze vikwazo vya kutosafiri na pia mali yao izuiliwe hadi hali iimarike.
WaandamanajiImage copyrightAFP
Image captionWaandamanaji nchini Gambia mapema mwaka huu
Kadhalika, wanataka taifa hilo litimuliwe kutoka kwa jumuiya ya miungano ya kanda.
Rais Jammeh aliingia madarakani kupitia mapinduzi ya serikali mwaka 1994.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment