Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, November 2, 2016

Ripoti ya Zuma kuhusu ufisadi yatolewa.

Maandamano yamekuwa yakifanyika kumtaka Zuma ajiuzulu

Image copyrightAFP
Image captionMaandamano yamekuwa yakifanyika kumtaka Zuma ajiuzulu
Idara ya kupambana na rushwa nchini Afrika Kusini imetoa ripoti iliyokuwa ikisubiriwa kuhusu uchunguzi kuwa familia tajiri ya Gupta ilikuwa na ushawishi mkubwa serikalini.
Ripoti hiyo inasema kuwa imetambua ushahidi unaoonyesha kuwa uhalifu huenda umefanyika katika viwango vya juu serikalini.
Imependekeza kuwa tume ya uchunguzi inayosimamiwa na hakimu ibuniwe ndani ya siku 30, kuchunguza madai ya ushawishi wa familia ya Gupta kwa uteuzi wa nyadhifa za serikali.
Tume hiyo mpya itawasilisha matokeo yake kwa rais ndani ya siku 180.
Ripoti hiyo pia inasema kuwa bwana Zuma alikuwa amevunja sheria ya kuzuia ufisadi kwa kushindwa kuchunguza madai kuwa watu wawili walipewa nyadhifa za uwaziri na familia ya Gupta.
Mtoto wa Zuma (kulia) alikuwa mshirika wa kibiashara na familia ya GuptaImage copyrightGALLO IMAGES
Image captionMtoto wa Zuma (kulia) alikuwa mshirika wa kibiashara na familia ya Gupta
Awali Rais Zuma alisitisha jitihada zake kwa njia ya mahakama, kuzuia kutolewa kwa ripoti iliyotengenezwa na Madonsela.
Madonsela alifanya uchunguzi kuhusu madai kuwa Zuma aliruhusu familia tajiri ya Gupta kuwa na ushawishi mkubwa serikalini.
Makundi ya upinzani yamekuwa yakifanya maandamano kwenye miji mkubwa nchini Afrika kusini kupinga uongozi wa rais Jacob Zuma.
Chanzo:BBC Swahili
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment