Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Friday, November 11, 2016

Picha tano za kusisimua mkutano wa Trump na Obama

Rais mteule wa Marekani Donald Trump alipokutana na Rais Barack Obama kwa mara ya kwanza ikulu ya White House tangu ashinde uchaguzi, uadui kati yao ulijidhihirisha.

Bw Trump kwenye kampeni alimweleza Bw Obama kama rais mbaya zaidi kuwahi kuongoza Marekani.
Rais Obama naye alisema Mwanarepublican huyo hana sifa na uwezo wa kuwa kiongozi wa Marekani.
Mfanyabiashara huyo tajiri kutoka New York, ambaye sasa ni rais mteule, kwa muda mrefu alitilia shaka uhalali wa habari kwamba Obama alizaliwa Hawaii, na alikejeliwa hadharani na Rais Obama.
Wawili hao walishauriana kwa zaidi ya saa moja afisi ya rais katika ikulu ya White House mnamo Alhamisi na walipojitokeza kwa wanahabari, walijaribu kuficha uadui kati yao.
Waliongea maneno mazuri kuhusu umoja na umuhimu wa kupokezana madaraka kwa amani.
Lakini picha zilizopigwa zinaonesha jambo tofauti, ukiangalia sura na mikono...
Trump na Obama wakiwa Oval OfficeImage copyrightREUTERS
Image captionNikiangalia sana pale mbali, haya masaibu yote yatapita...
Trump na Obama wakiwa Oval OfficeImage copyrightREUTERS
Image captionFikira za Trump zinaonekana kuyumba ... labda kwa kukumbuka aibu iliyotokana na utani kuhusu kuzaliwa kwa Obama mwaka 2011.
Trump na Obama wakiwa Oval OfficeImage copyrightEUROPEAN PHOTOPRESS AGENCY
Image captionWanasalimiana lakini macho yako wapi.... taama mdomo wa Trump
Trump na Obama wakiwa Oval OfficeImage copyrightAFP
Image captionTena, sasa Obama anamwangalia Trump.... lakini Trump anaamua, la hasha, SIWEZI kumwangalia machoni
Trump na Obama wakiwa Oval OfficeImage copyrightREUTERS
Image captionKupeana mikono kwisha sasa, na ni furaha sana kwa Trump .... lakini anaonekana kutoyaamini anayoyasema Rais Obama

Lakini yote hayakuwa kununa tu...
Trump na Obama wakiwa Oval OfficeImage copyrightEUROPEAN PHOTOPRESS AGENCY
Image captionWawili hao walicheka wakati mmoja walipotaniana.

Melania na Michelle pia walikutana, lakini hawakuonekana kuwa na matatizo
Melania Trump na Michelle ObamaImage copyrightWHITE HOUSE
Image captionMelania Trump na Michelle Obama wakiwa ikulu ya White House
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment