Writen by
sadataley
8:47 PM
-
0
Comments
KIONGOZI wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis amemteua Padre Edward Mapunda (51) kuwa Askofu Mpya wa Jimbo la Singida.
Akizungumza kwenye Ibada maalumu ya kumshukuru Mungu kwa uteuzi huo, Askofu Msimamizi wa Jimbo la Singida, Desderius Rwoma alisema kuwa taarifa ya uteuzi huo imetolewa na Balozi wa Papa hapa nchini, Askofu Mkuu Francisco Padilla.
Askofu Rwoma alisema kuwa jimbo hilo limepokea uteuzi huo kwa furaha kuu kutokana na ukweli kwamba kwa muda wa zaidi ya miaka mitatu halikuwa na askofu wa kudumu baada ya yeye kuhamishiwa Jimbo la Bukoba mkoani Kagera.
“Kutokana na uteuzi huo, jimbo sasa limeanza maandalizi kamambe ya kumpokea Askofu Mteule Mapunda na kufanya maandalizi ya kusimikwa kwake yanayotarajiwa mapema Julai mwaka huu,” alisema Askofu Rwoma.
Kwa mujibu wa Askofu Rwoma, Mapunda amekuwa kwenye nafasi ya upadre kwa muda wa miaka 19 sasa. Kwa wakati huu Padre Mapunda yuko masomoni Ireland na anatarajiwa kukamilisha masomo yake Juni mwaka huu.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments
Post a Comment