Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, June 3, 2015

China:Meli haikuweza kuzuia upepe mkali

Maafisa wa Uchina wanasema meli ndogo iliopatwa na ajali na kuzama katika mto Yangtse ikiwa na abiria zaidi ya 450 haikuwa na uwezo wa kuhimili dhoruba ya upepo mkali. Meli hiyo iitwayo The Eastern Star ilizama dakika chache tu ilipokumbwa na upepo uliovuma kwa kasi usiku wa Jumatatu. Miaka miwili iliyopita meli hiyo ilichunguzwa kwa madai ya kukiuka vigezo vya ubora na usalama. Hata hivyo maafisa wanasema kuwa hawajakata tamaa ya kuwapata watu walionusurika ajali ya meli na vikosi vya uokoaji vinaendelea kuwatafuta walionaswa ndani ya meli hiyo kwa siku ya pili. Watu saba wamethibitishwa kufariki huku watu kumi na tano wakiokolewa.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment