Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, June 3, 2015

Benitez ndio kocha mpya wa Real Madrid

Aliyekuwa kocha wa Napoli Rafa Benitez amethibitishwa kuwa k ocha wa Real Madrid katika kandarasi ya miaka mitatu. Benitez mwenye umri wa miaka 55 anachukua mahala pake Carlo Ancelotti ambaye aliondoka katika kilabu hiyo miezi 12 tu baada ya kuisaidia kushinda kombe lao la kumi la vilabu bingwa Ulaya. Benitez ambaye ni mzaliwa wa Madrid amehudumu misimu miwili kama mkufunzi wa Napoli ,baada kufanikiwa na vilabu kadhaa vya Ulaya. Baada ya kuisaidia Valencia kushinda kombe la Uefa mwaka 2004,mwaka unaofuatia alielekea Liverpool na kuisaidia kilabu hiyo kushinda kombe la vilabu bingwa ikiwa ni msimu wake wa kwanza katika kilabu hiyo ya Mersyside. Miaka miwili baadaye aliisaidia Liverpool kufika katika fainali za kombe la vilabu bingwa Ulaya na mwaka 2013 alikuwa kaimu mkufunzi wa Chelsea waliposhinda kombe la Yuropa.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment