Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Saturday, June 13, 2015

Afrika yatakiwa kutotegema misaada

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema wakati umefika kwa mataifa ya Afrika kukoma kutegemea misaada kutoka mataifa ya nje. Kwenye ujumbe alioutuma katika mtandao wake wa kijamii wa Twitter, rais Kenyatta amesema misaada hiyo ya kigeni mara nyingi huwa na vikwazo na masharti ambayo yanakandamiza. Ameongeza kusema kuwa hatma ya bara la afrika siku zijazo haipaswi kuwa mikononi mwa mataifa ya magharibi ambayo mara nyingi huweka maslahi yao kwanza. Kenya hutegemea mabilioni ya dola kila mwaka yanayotolewa na mataifa ya kigeni na katika bajeti ya mwaka wa 2015-16 waziri wa fedha wa Kenya alijumuisha misaada kutoka nje katika makisio ya serikali ya mwaka huu.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment