Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Thursday, April 2, 2015

NEC ITATOA RATIBA KAMILI KUHUSU BVR NA KURA YA MAONI – PINDA.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema kuwa serikali imeiagiza Tume ya Taifa ya Uchaguzi kutoa ratiba kamili kuhusu zoezi la uandikishwaji Wapiga Kura kwa BVR pamoja na hatma ya Kura ya Maoni ya Katiba Mpya. Pinda ameyasema hayo wakati akiahirisha Bunge majira ya saa 6 usiku wa kuamkia Alhamis tarehe 02 April, 2015 ambapo amedai kuwa tayari serikali imekwisha lipia pesa zote kwa ajili ya mashine zote za kuandikishia (BVR). “Serikali imekwishatoa pesa kwa ajili ya mashine zote za BVR kilichobaki ni kwa Tume kupanga ratiba yao, tuna imani kuwa mashine zote zikifanya kazi zoezi la uandikishwaji wapiga kura litamalizika kwa wakati” Amesema Pinda Amesema ameongea na Mwenyekiti wa tume hiyo leo (April 01) na imemuhakikishia kuwa itatangaza ratiba nzima kabla ya Pasaka. Kuhusu ugawaji wa Katiba Pendekezwa amesema kuwa tayari nakala 1,141,300 kwa upande wa Tanzania Bara na nakala 210,000 kwa upande wa Zanzibar zimekwisha sambazwa. Kuhusu muswada wa mahakama ya Kadhi, Pinda amesema serikali imefurahishwa na uamuzi wa muswada huo kuondolewa kwa kuwa itapata muda wa kutosha kujadiliana na wadau na kutoa elimu zaidi kuhusu umuhimu wa Mahakama hiyo. Bunge limeahirishwa hadi tarehe 12 Mei, 2015 kwa ajili ya mkutano wa 20 likiwa limejadili na kupitisha miswada 14 kati ya 21 iliyokuwa imepangwa katika mkutano huu uliomalizika leo. Kabla ya kuahirishwa, bunge limefanya maamuzi ya kupitisha muswada wa uhalifu wa kimitandao huku likiwa na wabunge wasiofikia nusu ya wabunge wote kama inavyotakiwa kwa mujibu wa kanuni.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment