Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, February 3, 2015

UVUKE KWAYA YAMSHUKURU MUNGU PAMOJA NA FAMILIA YA MALECELA.

Kwaya kongwe ya Uvuke kutoka Kanisa Kuu Anglikana Mkoani Dodoma ilipata wasaa wa kumtangaza Kristo pamoja na baadhi ya viongozi wa chama na serikali waliojumuika katika tafrija fupi ya kumpongeza Mheshimiwa Anne Kilango Malecela kwa kuteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Elimu katika sherehe ambayo ilifanyika nyumbani kwa Waziri Mkuu mstaafu na mbunge wa Mtera Mheshimiwa mzee John Malecela ambaye pia ni mlezi wa kwaya hiyo inayosifika kwakuimba kwa ustadi wa hali ya juu nyimbo zenye mahadhi ya kabila la Wagogo nchini.

Kati ya viongozi waliohudhuria sherehe hiyo ni pamoja na mheshimiwa Hezekiah Chibulunje, Job Ndugai, Samwel Sitta na mkewe Margaret Sitta, wakuu wa wilaya Bahi na Chamwino pamoja na baadhi ya wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Baadhi ya picha zikionyesha mheshimiwa John Malecela akiwa na wanakwaya wa Uvuke nyumbani kwake mjini Dodoma.



        Picha za chini kwaya hiyo ikiwa katika mwaliko mwingine wa kihuduma hapo jana
Add caption




Safu ya wanamuziki wa Uvuke Choir Dodoma ©Uvuke Choir
    Chanzo: Gospelkitaa.co.tz
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment