Writen by
sadataley
5:59 PM
-
0
Comments
Dar es Salaam.Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imewataka viongozi wa dini kutumia nafasi kukemea juu ya matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii kwa waumini wao na kuelimisha madhara yanayoweza kusababishwa na teknolojia hiyo katika jamii.
Hatua hiyo ya TCRA imekuja kufuatia kukithiri kwa vitendo vinavyoashiria kutumika vibaya kwa mitandao ya kijamii kama njia ya mawasiliano hali inayochangia kuzidi kuporomoka kwa maadili.
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Profesa John Nkoma alisema lengo la kukutana na viongozi hao ni kuwapa elimu kuhusiana na madhara ambayo jamii inaweza kupata kufuatia ongezeko la matumizi mabaya ya mitandao.
“Mitandao ni mizuri sana lakini tatizo ni jinsi inavyotumika watu wamekuwa wakifanya mambo ya ajabu tena bila kuwa na hofu ya Mungu ndiyo maana tumerudi kwenu viongozi wa dini mtusaidie katika hili:
Kwa kutumia nafasi zenu tuna imani mtawaelimisha waumini ili waelewe kuwa kusambaza ujumbe unaoashiria uchochezi ni kosa kisheria na inaweza kuwa dhambi kwani hakuna ambaye angependa amani ivunjike”
Katika miaka ya hivi karibuni baada ya kuboreshwa na kurahisishwa kwa teknolojia ya mawasiliano watu wamekuwa wakitumia mwanya huo kusambaza meseji na picha za matusi na zinazolenga kuleta uchochezi.
Alisema ili kuepukana na madhara inawalazimu watanzania kuachana na matumizi mabaya ya mitandao na badala yake kuitumia katika kuleta maendelea kwenye sekta mbalimbali ikiweo elimu,biashara na uchumi.
“Vijana watumie mitandao kujifunza mambo mbalimbali yanayoweza kuwa na manufaa kwao na taifa lakini sio kuhamasishana vitu vya ajabu”alisema.
Kwa upande wake Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhadi Mussa Salum aliwataka watanzania kuwa makini na matumizi ya mitandao na kusisitiza kwamba inaweza kusababisha madhara makubwa kwa taifa.
Naye Msaidizi wa Askofu Kanisa la KKKT huku akiwasisitiza kuzingatia hofu ya Mungu katika kila wanalofanya hali itakayowaweka mbali na vitendo viovu.
Chanzo: MWANANCHI
Chanzo: MWANANCHI
No comments
Post a Comment