Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Monday, February 2, 2015

Rais Salva Kiir na Riek Machar watia saini mkataba

 Rais Salva Kiir wa Sudan kusini (kushoto)  mpinzani wake  Riek MacharRais wa Sudan Kusini Salva Kiir na kamanda wa waasi Riek Machar wamesaini makubaliano ya kumaliza mzozo ambao umegubika na kuharibu nchi yao.
Makubaliano hayo ya kusitisha mapigano yalitiwa saini Jumatatu mjini Addis Ababa Ethiopia kwa msaada wa wapatanishi kutoka  Jumuiya ya maendeleo ya serikali za kanda ya Afrika Mashariki IGAD.
Hakuna upande uliotoa maelezo ya kina kuhusu makubaliano hayo lakini wamesema watakutana tena Februari 20 kukamilisha maswala yote kwenye mkataba huo.
Wote, Kiir na Machar wametia saini mikataba mingine hapo awali lakini ikavunjika. Mpatanishi wa IGAD Seyoum Mesfin alionya kuwa yeyote atakayevunja makubaliano  yaliyotiwa saini hivi karibuni, ataripotiwa kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment