Writen by
sadataley
5:29 PM
-
0
Comments
RAIS wa Zimbabwe Robert Mugabe, 90, ameanguka akishuka kwa kutumia ngazi baada ya kuhutubia wafuasi wake kwenye jukwaa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Harare.
Kiongozi huyo alikuwa tu amewasili Zimbabwe kutoka Ethiopia ambako alitawazwa mwenyekiti wa Muungano wa Afrika.
Kiongozi huyo mkongwe zaidi Afrika, na atakayetimu miaka 91 baadaye mwezi huu, alikuwa amekamilisha kutoa hotuba yake ya kurudi nyumbani alipoanguka kwenye ngazi, kisa kilichoshuhudiwa na wanahabari na wafuasi wengi.
Alisaidiwa upesi kuamka na wasaidizi wake ambao walimwingiza kwenye gari lililokuwa karibu.
Mugabe alichukua uongozi wa AU Ijumaa, akichukua wadhifa huo kutoka kwa Rais wa Mauritania Mohamed Ould Abdel Aziz.
Ndiyo kiongozi wa tatu kwa kukaa zaidi uongozini Afrika.
No comments
Post a Comment