Writen by
sadataley
7:14 PM
-
0
Comments
Na Sharon Sauwa, Mwananchi
Dodoma. Moto wa uchaguzi mkuu umezidi kupamba baada ya mtandao wa walimu vijana nchini kujitokeza hadharani na kuahidi kumpigia kampeni Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba katika safari yake ya kuwania urais.
Pia, mtandao huo uliahidi kuwafanyia kampeni
Makamba na vijana wenzake wote watakaojitokeza kuwania ngazi mbalimbali
za uongozi bila kujali itikadi za vyama vyao iwe CCM, Chadema,
NCCR-Mageuzi au chama kingine chochote hadi ndoto yao ya vijana
kujiongoza na kujitawala itakapotimia.
Walimu hao walikusanyika jana katika Ukumbi wa
Shule ya Sekondari ya Umonga mjini Dodoma pamoja na kuzindua uanzishwaji
wa mtandao huo, walitangaza kumuunga mkono Makamba.
Akisoma tamko la mtandao huo, Mwenyekiti wake,
tawi la Dodoma, Fredrick Mwakisambwe, alisema mtandao huo, unamuunga
mkono Makamba kwa sababu ni mzalendo, mwadilifu na ana uwezo kuongoza.
“Na tunawahimiza na kuwahamasisha vijana wengine
wengi zaidi wajitokeze kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ikiwamo
uenyekiti wa Serikali za Mitaa, vijiji, udiwani na ubunge.”
Alisema ni wajibu wao kuwakumbusha Watanzania
kwamba Taifa hili lilikombolewa na ndio maana kiongozi wa kwanza wa
Taifa hili alikuwa mwalimu tena kijana akiwa na umri wa miaka 39 tu.
Sisi walimu vijana kupitia huu mtandao wetu bila
kuuma maneno tunasema tunataka Taifa letu liongozwe sasa na kiongozi
mwenye kuendana na changamoto za kizazi hiki, mwenye fikra za hiki
kizazi,” alisema
No comments
Post a Comment