Writen by
sadataley
7:04 PM
-
0
Comments
Na Florence Majani,Mwananchi
Dar es Salaam. Shirika la Polisi la Kimataifa (Interpol), Tawi la Tanzania, limemhoji kwa saa kumi na moja binti aliyerubuniwa na kupelekwa China ambako kwa miezi mitatu alikuwa akitumikishwa kwenye madanguro nchini humo.
Siku chache zilizopita, gazeti hili liliandika
mfululizo, makala kuhusu msichana Munira Mathias, (si jina lake halisi)
aliyetumikishwa kwenye madanguro nchini China, baada ya kurubuniwa
kwamba alikuwa akipelekwa kufanya kazi kwenye hoteli kubwa.
Munira alisema baada ya taarifa zake kuandikwa na
gazeti hili Interpol walimtaka afike ofisini kwao kwa mahojiano. Mara ya
kwanza alihojiwa kwa saa saba na aliitwa tena mara ya pili na kuhojiwa
kwa saa tatu na nusu.
“Walinihoji jinsi safari yangu ilivyokuwa na namna
ambavyo wale wanawake waliotuchukua kutoka hapa (Tanzania) hadi China
na walivyosuka mipango ya kunisafirisha,” alisema.
Alisema: “Walikuwa wanataka kuendelea kufahamu kwa
kina jinsi nilivyosafirishwa na walionisafirisha, hata hivyo nimewapa
ushirikiano wa kutosha.”
Mkuu wa Interpol Tawi la Tanzania, Kamishna
Msaidizi wa Polisi (ACP), Gustav Babile alikiri ofisi yake kumhoji
Munira na kwamba lengo ni kufahamu kwa undani jinsi Watanzania
wanavyotumikishwa kwenye madanguro hayo, pamoja na kujua jinsi biashara
ya binadamu kati ya China na Tanzania inavyofanyika.
“Nia ilikuwa ni kujua namna wasichana
wanavyotolewa hapa na kupelekwa huko, lakini kikubwa ni kufanya kazi
yetu kukomesha biashara hiyo kimataifa,” alisema Babile.
Alisema siyo mara ya kwanza kwa Interpol kufanya
jitihada za kukomesha biashara ya binadamu na kwamba hatua zimekuwa
zikichukuliwa kila mara na siyo kwa Watanzania pekee, bali hata raia wa
kigeni wanaokuja nchini.
“Tunafanya hii operesheni mara kwa mara. Kwa
mfano, waliwahi kuletwa wanawake kutoka Nepal, walipofika hapa hati zao
za kusafiria zikafichwa na wale wanaowatumikisha na wakaanza kufanya
biashara ya ukahaba na baadaye kuwalipa wale waliowaleta,”alisema
Babile.
Alisema kitengo hicho kimewahi kuwarudisha wanawake kutoka China waliofika hapa nchini kwa nia ya kufanya biashara ya ukahaba.
Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Lucy Ngonyani ambaye
ndiye aliyemhoji Munira alisema wanaendelea kufanya uchunguzi wa kina
kuhusu tukio la binti huyo kupelekwa China na matukio mengine yenye
uhusiano au kufanana na hilo.
Kwa habari zaidi ingiahttp://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-Aliyetumikishwa-China-ahojiwa-/-/1597296/2391518/-/rbds8qz/-/index.html
Kwa habari zaidi ingiahttp://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-Aliyetumikishwa-China-ahojiwa-/-/1597296/2391518/-/rbds8qz/-/index.html
No comments
Post a Comment