Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Friday, July 11, 2014

HIZI NDIZO NYIMBO 10 ZA INJILI HUIMBWA ZAIDI DUNIANI


Mwanamama Darlene Zschech.
Jarida maarufu duniani liitwalo Christian Music, Christ Magazine au CCM kama linavyofahamika zaidi, limetoa orodha ya nyimbo 10 za injili ambazo zimeonekana kuwabariki watu wengi sana duniani toka zilipotoka kwa mara ya kwanza.

Kati ya nimbo hizo ni pamoja na Shout to The Lord utunzi wake mwanamama Darlene Zschech, El Shaddai wa kwake mwanamama Amy Grant, Cinderella wa kwake Steven Curtis Chapman, 10,000
Nikiwa nimepozi na mwanamama Amy Grant.
Reasons wa kwake Matt Redman, Awesome God wake Rich Mullins, Jesus Freak  wao dc talk, Friends utunzi wake Michael W Smith, I can only imagine utunzi wake MercyMe, Flood wa kwao Jars of Clay pamoja na Revelation Song wa kwake Jennie Lee Riddle.
Kwa mujibu wa jarida hilo ambalo limetoa nyimbo hizo kwa mujibu wa utafiti wao likiwa linasherehekea miaka 35 toka lilipoanza kuchapishwa, limeandika kwamba nyimbo hizo ndio zinaimbwa sana makanisani, na kuongeza kwamba wimbo Shout to The Lord ambao hushusha uwepo wa Mungu kwakusifu ama kuabudu umeimbwa na watu takribani milioni 30 wanaohudhuria kanisani kila wiki, ukiwa pia umeimbwa mbele ya Rais wa Marekani pamoja na Papa.

Kwa upande wa Darlene ameonyesha moyo wa shukrani kwa Mungu hasa baada ya wimbo wake kuwemo kwenye orodha hiyo, huku watu wengi pia wakieleza namna walivyompokea Yesu kupitia wimbo wake.

Nikiwa na Matt Redman mtunzi wa wimbo mwingine maarufu wa 'Heart of Worship' nilipokutana naye kwenye kambi ya vijana maarufu nchini Uingereza ya Soul Survivor.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment