Writen by
sadataley
1:19 PM
-
0
Comments
Mji wa Ninawi uonekanavyo kwasasa. |
Yona 3
1 Neno la Bwana likamjia Yona mara ya pili, kusema,
2 Ondoka, uende Ninawi, mji ule mkubwa; ukaihubiri habari nitakayokuamuru.
3 Basi
Yona akaondoka, akaenda Ninawi, kama Bwana alivyonena. Basi Ninawi
ulikuwa mji mkubwa mno, ukubwa wake mwendo wa siku tatu.
4 Yona akaanza kuuingia mji mwendo wa siku moja, akapaza sauti yake, akasema, Baada ya siku arobaini Ninawi utaangamizwa.
5 Basi
watu wa Ninawi wakamsadiki Mungu; wakatangaza kufunga, wakajivika nguo
za magunia, tangu yeye aliye mkubwa hata aliye mdogo.
6 Habari ikamfikia mfalme wa Ninawi, naye akaondoka katika kiti chake cha enzi, akavua
Ramani inayoonyesha mji wa Ninawi ulipo. |
vazi lake, akajivika nguo za magunia, na kuketi katika majivu.
7 Naye
akapiga mbiu, akatangaza habari katika mji wa Ninawi, kwa amri ya
mfalme na wakuu wake; kusema, Mwanadamu asionje kitu, wala mnyama wala
makundi ya ng'ombe, wala makundi ya kondoo; wasile, wala wasinywe maji;
8 bali
na wafunikwe nguo za magunia, mwanadamu na mnyama pia, nao wakamlilie
Mungu kwa nguvu, naam, na wageuke, kila mtu akaache njia yake mbaya, na
udhalimu ulio mikononi mwake.
9 Ni nani ajuaye kwamba Mungu hatageuka na kughairi, na kuiacha hasira yake kali, ili msiangamizwe?
10 Mungu
akaona matendo yao, ya kuwa wameiacha njia yao mbaya. Basi Mungu
akalighairi neno lile baya, ambalo alisema atawatenda; asilitende.
Mji wa Ninawi upo mashariki ya kati nchini Iraki. Mji huo unaoaminika kukaliwa na Wakristo wengi upo kilometa 400 kaskazini magharibi mwa Iraki, ingawa toka vita ilipoingia ya kumuondoa aliyekuwa Rais wa nchi ya Iraki marehemu Saddam Hussein, inaelezwa idadi ya Wakristo katika mji huo imepungua kwasababu baada ya mji mkuu wa Mosul kutekwa na waislamu wenye msimamo mkali wanaojiita Islamic state ama Isis zamani wakitambulika hivyo, kumewafanya wakristo wengi kuukimbia mji wa Mosul ambao majengo yake ni ya kisasa zaidi kulinganisha na Ninawi.
Watoto wakicheza nje ya nyumba zao huko Ninawi©nationalgeographical. |
Mwishoni mwa wiki iliyopita wakristo waliamliwa kuondoka katika mji wa Mosul, tamko lililotolewa na wanajeshi wa Sunni (moja ya majeshi makubwa ya kiislamu) na mpaka kufikia jumamosi iliyopita wakristo wengi waliamua kuhama mji huo na kukimbilia miji ya karibu inayokaliwa na wakristo, kwa mujibu wa ripoti kutoka vyombo vya habari vya kimataifa vinasema wakristo waliamua kuondoka Mosul wakiacha samani zao nyuma na kuondoka na nguo walizovaa tu na kukimbilia kijiji cha Al Qosh mji mkubwa wa wakristo ambao unadaiwa kabla majeshi hayo ya kiislamu kuchukua mji ulikuwa na wakristo wafikao 30,000 lakini toka june mwaka huu wakristo waliosalia waliamua kuukimbia mji. (Popote ulipo maombi yako ni muhimu sana kwa ndugu zetu hawa).
Lango la kuingilia mji wa Ninawi lionekanavyo kwasasa©atlastours. Habari kwa hisani ya Mtandao wa Gospel Kitaa |
No comments
Post a Comment