Writen by
sadataley
4:58 PM
-
0
Comments
Afisa mmoja mwandamizi katika wizara ya maswala ya kigeni nchini Sudan amesema kuwa mwanamke aliyepewa hukumu ya kifo kwa kubadili dini yake ya kiislamu,Meriam Ibrahim atawachiliwa huru katika kipindi cha siku chache zijazo.
Abdullahi Alzareg ambaye ni katibu katika wizara hiyo amesema kuwa Sudan inatilia maanani uhuru wa kuabudu na kwamba serikali itamtetea mwananmke huyo.
Kumekuwa na shutma za kimataifa kuhusu hukumu aliyopewa mwanamke huyo.
Meriam Ibrahim anazuiliwa katika jela moja ambapo alijifungua mtoto wa kike juma hili.
Ameolewa na mkristo na pia amehukumiwa kuchapwa viboko mia moja kwa kuzini kwa sababu mwanamke wa kiislamu kuolewa na mkristo ni haramu kulingana na sheria za Sudan.
chanzo BBC Swahili.
Soma HAPA ZAIDI
Daniel akiwa amembeba motto wake aliyezaliwa wiki iliyopita. |
Meriam akiwa amebeba motto wake aliyejifungua huko gerezani |
Meriam na mumewe, pembeni mtoto wao wa kiume anayeishi naye jela. HABARI NA GOSPEL KITAA |
No comments
Post a Comment