Writen by
sadataley
4:29 PM
-
0
Comments
Na Daniel Mjema, MwananchiDodoma. Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni (KUB), Freeman Mbowe amemtunishia misuli, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisema hawatishwi na kusudio alilotoa la kubadili kanuni ili kudhibiti tabia ya kambi hiyo kususia vikao vya Bunge kila wanapopinga hoja.
Mbowe alisema jana mjini hapa kwamba, wako tayari kwenda jela na hata ikibidi kufa kwa kupambana na ufisadi ndani ya Serikali.
Pinda alitoa pendekezo hilo baada ya wabunge wa
upinzani ambao pia ni wanachama wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa),
kususia Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini na kutoka bungeni.
Baada ya kupitishwa kwa bajeti ya wizara hiyo,
Pinda alipendekeza kubadilishwa kwa kanuni ili kuwadhibiti wabunge wa
upinzani kutoka nje ya Bunge mara kwa mara.
“Inawezekana kanuni zinaruhusu... lakini
haiwezekani kila mnaposhindwa hoja muone njia rahisi ni kutoka nje,
nasema hivi, Watanzania hawawezi kukubaliana na hili,” alisema Pinda
Ijumaa iliyopita na kuongeza:
“Tabia hii inayoendelea kujengeka siyo nzuri.
Tuombe kanuni za Bunge zirekebishwe kwa sababu Bunge linaonekana halina
watu wakati hao waliotoka hawana sababu za msingi.”
Akizungumzia pendekezo hilo, Mbowe ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Chadema alisema wabunge wa kambi hiyo wako tayari kupokea
adhabu yoyote itakayotokana na kubadilishwa kwa kanuni za kudumu za
Bunge hilo.
“Katika kutafuta haki, ustawi na heri ya taifa
letu na ya vizazi vijavyo vya nchi yetu, tuko tayari siyo tu kukabili
adhabu zitakazotokana na kubadilishwa kwa kanuni, bali hata kwenda jela
na kufa.
“Ni heri kufa umesimama kwenye haki kuliko kuishi ukiwa umesimama kwenye ubatili.
Tunafahamu gharama na mateso tunayopitia kwa ajili
ya kupinga ufisadi na ubadhirifu. Tumeamua kupambana mpaka mwisho
hatimaye haki na ukweli vitatuweka huru.”
Baada ya kususia Bunge Ijumaa iliyopita, Mbowe
alikutana na waandishi wa habari na kudai kuwa kulikuwa mkakati mahususi
wa kuwazomea na kuwatukana.
“Tulitambua kwamba kuna mkakati mkubwa
ulioandaliwa baina ya Serikali, uongozi wa Bunge na wabunge wa CCM
kujaribu kufukia ufisadi mkubwa ambao unaikumba ya Wizara ya Nishati na
Madini,” alisema Mbowe.
Kwa habri za kwa kinaiga http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Mbowe-amtunishia-misuli-Waziri-Mkuu/-/1597296/2334478/-/nvmf6c/-/index.html
Kwa habri za kwa kinaiga http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Mbowe-amtunishia-misuli-Waziri-Mkuu/-/1597296/2334478/-/nvmf6c/-/index.html
No comments
Post a Comment