Writen by
sadataley
4:27 PM
-
0
Comments
Na Waandishi Wetu, Mwananchi
Dar es Salam na Morogoro. Mtoto Nasra Rashid
Mvungi (4), aliyefichwa kwenye boksi kwa miaka minne, amefariki dunia
katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na katika saa zake za mwisho
za uhai wake alisikika akitamka maneno “sitaki waje kunichukua”.
Nasra ambaye alikuwa akitibiwa MNH, alifariki
dunia usiku wa kuamkia jana baada ya hali yake kubadilika Alhamisi
iliyopita, kiasi cha kuhamishiwa katika chumba cha uangalizi maalumu
(ICU) ambako aliwekewa mashine ya kumsaidia kupata hewa ya oksijeni.
Mama mlezi wa Nasra, Josephine Joel alisema kabla
hajawa mahututi, mtoto huyo alikuwa akiweweseka kwa kuzungumza maneno
mengi hali iliyosababisha wauguzi kumfanyia ibada maalumu.
“Sitaki waje kunichukua, sitaki, sitaki, wasije
kunichukua, bibi Nasra umesikia,” ni maneno aliyokariri mlezi huyo
ambayo yalikuwa yakirudiwarudiwa na Nasra saa chache kabla ya hajawa
mahututi na kupelekwa ICU.
Josephine alisema mtoto huyo pia kila mara alikuwa
akidai apewe chips na soda na kwamba hadi mauti yalipomkuta alikuwa
akitibiwa maradhi ya homa ya mapafu ‘nemonia’.
“Nasra alifariki saa 7.30 usiku, tangu Alhamisi
iliyopita hali yake ilibadilika na kuwa mbaya na imeendelea kuwa hivyo
hadi alipofariki dunia,” alisema na kuongeza:
“Bado niko Muhimbili nawasubiri watu wa ustawi wa
Jamii kutoka Morogoro wao ndiyo watakuwa na uamuzi kuhusu mazishi ya
mtoto huyo,” alisema.
Ofisa Habari wa MNH, Aminiel Eligaeshi
alithibitisha kifo cha mtoto huyo, ambaye alipokewa hospitalini hapo Mei
26 mwaka huu akitokea Morogoro na kwamba hali yake ilibadilika ghafla
juzi saa 2:00 usiku.
“Jitihada za madaktari zilifikia kikomo saa 7:30 usiku, baada ya mtoto huyo kupoteza maisha,” alisema.
Kuzikwa kishujaa
Ofisa ustawi wa jamii Mkoa wa Morogoro, Oswin Ngungatuti alisema mwili wa mtoto huyo utasafirishwa leo kwenda Morogoro.
Ngungamtitu alisema mazishi ya Nasra yatatanguliwa
na ibada itakayoambatana na utoaji wa heshima za mwisho katika Uwanja
wa Jamhuri, hatua ambayo alisema inatokana na baba mzazi wa mtoto huyo,
Rashid Mvungi kuwa mmoja wa watuhumiwa wa mateso yake.
Kwa habari kwa kina ingiahttp://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Kauli-ya-mwisho-ya--mtoto-wa-boksi--/-/1597296/2334496/-/p0w957z/-/index.html
Kwa habari kwa kina ingiahttp://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Kauli-ya-mwisho-ya--mtoto-wa-boksi--/-/1597296/2334496/-/p0w957z/-/index.html
No comments
Post a Comment