Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Saturday, February 15, 2014

Rais Kikwete: Kuna majangili papa 40 nchini

Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete akizungumza na mtangazaji wa kituo cha  televisheni cha  CNN, Christiane Amanpour jijini London. Picha na Ikulu 
Na Waandishi wetu, Mwananchi
Dar es Salaam/Arusha. Wakati kuna joto la vyombo vya habari vya kimataifa kuituhumu Tanzania kuwa haipambani na ujangili, Rais Jakaya Kikwete amesema Serikali imeubaini mtandao unaojumuisha watu 40, akiwemo tajiri maarufu mkoani Arusha.
Akihojiwa juzi jioni na Idhaa ya Kiswahili ya BBC, Rais Kikwete alikanusha taarifa zilizotolewa na gazeti la Sunday Mail la Uingereza zilizodai Tanzania haijafanya juhudi za kupambana na ujangili wa meno ya tembo, akisema taarifa hizo ni uzushi na upuuzi mtupu.
“Gazeti hilo limezungumza na nani, ndiyo maana sitaki kupoteza muda kujadili upuuzi, achana na mambo hayo. Ndiyo maana tunasema, akutukanaye hakuchagulii tusi,” alisema Rais Kikwete.
Alisema inashangaza kuona watu wanaozusha taarifa hizo hawaoni jinsi tulivyofanya jitihada za kutokomeza ujangili, kama operesheni za tokomeza ujangili na operesheni kipepeo.
Kuhusu majangili 40 ambao wametambuliwa, Rais Kikwete alisema wameutambua mtandao mkubwa wa majangili unaoongozwa na mfanyabiashara mkubwa wa Arusha Mjini.
“Kuna majangili 40 waliotambuliwa na tumetambua mtandao mzima, pale Arusha kuna mtu mkubwa alikuwa anaendesha biashara. Kazi ilikuwa ni kutambua mtandano wote, ule mtandao ni mpana sana,” alisema Rais Kikwete.
Katika mahojiano hayo, Rais Kikwete alisema, Tanzania ilikuwa ni nchi yenye tembo wengi zaidi duniani, lakini ujangili ulipokithiri, tembo walipungua na kufikia 57,000 tu mwaka 1987.
“Mwaka 1989, Taasisi ya Kimataifa ya Cites, walipiga marufuku biashara ya meno ya tembo duniani na ujangili ulipungua kwa kiasi kikubwa hivyo tembo waliongezeka na kufikia, 110,000 mwaka 2009,” alisema.
Kikwete ahojiwa CNN
Rais Jakaya Kikwete amekiri kuwa vita dhidi ya ujangili ni tatizo sugu linaloielemea Tanzania.
Wakati idadi ya tembo ikiendelea kupukutika kila siku, vita dhidi ya ujangili ilichukua sura mpya mwishoni mwa mwaka jana baada ya operesheni iliyofahamika kwa jila la Tokomeza Ujangili, kukumbwa na kashfa ya ukiukwaji wa haki za binadamu na kusababisha mawaziri wanne kujiuzulu.
Mawaziri waliojiuzulu ni pamoja na aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi, aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha na aliyekuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Dk David Mathayo.
Kwa habari zaidi ingia www.mwananchi.co,tz
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment