Writen by
sadataley
4:12 PM
-
0
Comments
![]() |
Mwangalizi mkuu wa vituo vya maombezi na ushauri, BCIC, Askofu Sylvester Gamanywa |
Mtandao wa vikundi vya maadili na uchumi tanzania. UVIMAUTA hatimaye kuzinduliwa rasmi Jumamosi hii, ambapo ni kilele cha mchakato wa uchumi wa kumilikisha kitakuwa siku hiyo, tarehe 15 Februari 2014, kuanzia saa tatu na nusu asubuhi hadi saa saba mchana kwenye ukumbi wa BCIC Mbezi Beach uliopo barabara ya Bagamoyo.
Akizungumza kwenye kipindi maalumu kupitia kituo cha WAPO Radio FM, askofu Gamanywa anasema mara baada ya uzinduzi, kinachofata ni utekelezaji.
Aidha askofu Gamanywa anaeleza namna ya uanachama utakavyokuwa, ya kwamba ni ndani ya vikundi vya watu 3-20 ndio wanaweza kuwa wanachama kwenye mtandao huu, ambapo pia muundi wa mtandao huu uko katika mfumo pekee wa kisayanssi, kwa maana ya kukua na kujizalisha wenyewe, tofauti na mitandao mingine. Unapokuwa umeanza, kampeni zinapomalizika, ni mwanzo wa kila mwanachama kuongoza kikundi kipya hadi vijijini. Yaani kila kikundi kinakuwa na maarifa ya kuanzisha kikundi kipya, na kadha na kadha, hadi kwenu.
Tofauti nyingine ambayo askofu Gamanywa anaeleza ni kwamba huu ndio mtandao pekee ambaop umetanguliza maadili, ili kudhibiti ufisadi, ndio maana vimetiwa kwa jina hilo, kwa kuwa vinakutana si tu kwa ajili ya kuzalisha, bali pia kuinuana kimaadili. Halikadhalika, vikundi vya mtandao huu vinakwenda kwa mfumo unaofanana, kwa maana ya hali ya kiuchumi, kimazingira, kijinsia, kiumri, na kadha wa kadha. kwa mfano, vijana wa kike, vijana wa kiume, vijana wenye vipaji, na kadha wa kadha.
Watu zaidi ya 2000 wameelezwa kujaza fomu hadi hivi sasa, ambapo wataalamu wanaendelea kujaza taarifa kwenye mitambo ili kupata namna ya kuunda vikundi, ambapo vikundi takriban 70 vimeshajulikana, huku idadi ya vikundi hivyo ikiendelea kuongezeka, huku tovuti ya mtandao huo nayo ikiwekwa sawa kwa ajili ya kufanya usajili.
Uzinduzi wa mtandao huu ni mwendelezo wa mkakati wa kueneza maadili kwa kizazi kipya, ambao Mheshimiwa Rais alizindua mnamo mwaka 2010
Habari na Gospel Kitaa
No comments
Post a Comment