Writen by
sadataley
11:43 AM
-
0
Comments
Maafisa wa Misri wanasema kuwa kumetokea mlipuko mkubwa wa bomu nje ya Makao makuu ya polisi jijini Cairo ambapo watu wanne wamefariki na wengine zaidi ya 70 kujeruhiwa.
Kituo cha televisheni cha Serikali kimesema kuwa milio ya risasi ilisikika mara tu baada ya mlipuko huo.
Moshi ulionekana ukifuka juu ya majengo katikati mwa mji na picha za televisheni zilionyesha uharibifu mkubwa wa majengo hayo.
Zaidi ya ambulansi 30 zimepelekwa eneo hilo kushughulikia waathiriwa. Mlipuko huo umetokea siku ya kuadhimisha miaka mitatu tangu kupinduliwa kiongozi wa nchi hiyo Hosni Mubarak.
No comments
Post a Comment