Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Sunday, January 12, 2014

Israel yaomboleza kifo cha Sharon

Watu nchini Israel leo wanaanza kipindi kifupi cha maombolezi kufuatia kifo cha waziri mkuu wa zamani Ariel Sharon aliyefariki akiwa na umri wa miaka 85 baada ya miaka 8 ya kuwa hali mahututi.
Wapalestina wakisherehekea kifo cha Ariel Sharon
Wananchi watatoa heshima zao za mwisho kwa mwili wake Jumapili kabla ya kuzikwa Jumatatu.
Viongozi wa dunia wametoa rambi rambi zao kwa Sharon, mtu aliyepigana katika vitaa vikuu vinne kabla ya kuingia katika ulingo wa siasa.
Lakini aliwaacha wapalestina wengi waliomuona kama adui wao wakiwa na hamaki.
Mkuu wa kituo cha afya cha Sheba mjini Tel Aviv alithibitisha kifo cha Sharon, Jumamosi mchana siku ya Sabato kwa wayahudi, zaidi ya wiki moja baada ya taarifa kutolewa kuhusu afya yake kuzorota.
Mmoja wa wanawe Sharon,Sharon, Gilad Sharon, alisema kuwa babake amekwenda wakati alipoamua mwenyewe kwenda.
Rais wa Marekani Barack Obama na mkewe Michelle Obama, wamesema Sharon, alikuwa kiongozi aliyejitolea kuwahudumia watu wa Israel.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment