Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Sunday, January 26, 2014

HABARI NJEMA KWA WAPENZI WA KUNDI LA GLORIOUS WANARUDI TENA KILA IJUMAA



Baada ya kupumzika kwa takribani miaka miwili toka wasimamishe ibada za kusifu na kuabudu siku za Ijumaa jioni, kundi la Glorious Worship Team (GWT) chini ya kiongozi wake Emanuel Mabisa kundi hilo limetangaza kuanza upya tena ibada hizo kuanzia ijumaa ya kwanza ya mwezi wa pili mwaka huu ingawa bado hawajatangaza mahali watakapokuwa wakifanyia maonyesho hayo awali kabla ya kusimamisha walikuwa wakifanyia katika ukumbi wa hoteli ya Atriums iliyopo Sinza jijini Dar es salaam.
Glorious ambao ni kundi la kwanza la muziki wa injili nchini kuamua kuwa na siku maalumu ya kuwakusanya mashabiki na wapenzi wa muziki wa injili kwa pamoja kila siku za ijumaa jioni ili kumsifu Mungu, kuchangamka na kucheza pamoja huku kundi hilo likisimamia ratiba nzima, utaratibu huo ulitokea kuanza kupendwa na wapendwa wengi ambao walikuwa wakiishia kujifungia ndani ya nyumba zao mpaka jumapili ndipo waende kanisani na kujikuta wakipata sehemu ya mtoko ambao hata hivyo ulikuja kusimama na sasa unarejea tena.

GWT mpaka sasa in a album mbili ya kwanza ilikuwa Niguse na yasasa iitwayo Umenifanya ibada. Angalia video ya chini kama walivyonaswa katika moja ya huduma zao walipotembelea jijini Mwanza. Video hii si rasmi bali mmoja wa waliohudhuria alirekodi wimbo huu.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment