Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Saturday, November 23, 2013

WAZIRI WA NISHATI AFANYIWA MAOMBI OFISINI KWAKE

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akiwa amepiga magoti kama ishara ya unyenyekevu huku akiwa amewekewa mikono na viongozi kutoka madhehebu mbalimbali waliokuwa wakimwombea ofisini kwake.
Baadhi ya viongozi wa madhehebu mbalimbali wakisaini kitabu cha wageni kwenye ofisi ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo kabla ya kuanza kwa kikao chao. Viongozi hao walifika kwa ajili ya kumpongeza Waziri Muhongo kwa kazi nzuri ikiwa ni pamoja na kumfanyia maombi maalumu.
Viongozi kutoka madhehebu mbalimbali wakiendelea kubadilishana mawazo mara baada ya kumaliza kikao chao na Waziri. Aliyesimama ni Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akiagana na baadhi ya viongozi wa madhehebu mbalimbali mara baada ya kumalizika kwa kikao.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ( wa sita kutoka kushoto) na Naibu Katibu Mkuu wa Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava ( wa pili kutoka kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi kutoka madhehebu mbalimbali mara baada ya kumalizika kwa kikao. Picha kwahisani ya Issamichuzi.blog
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment