Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Monday, November 25, 2013

Wazazi wamsindikiza Zitto ‘kujieleza’

Wazazi wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, Mzee Kabwe Zuberi na Shida Salum. 
Na Freddy Azzah, Mwananchi
Dar es Salaam. Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe,  jana alisindikizwa na wazazi wake pamoja na wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya katika mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari aliouitisha baada ya kuvuliwa nyadhifa zake zote ndani ya chama hicho. Tangu alipoanza kupata umaarufu katika medani ya siasa, mbunge huyo hajawahi kuonekana hadharani akiwa na baba yake mzazi, Zuberi Kabwe, bali mama yake Shida Salum ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema.
Mbali ya wazazi hao, wasanii maarufu waliokuwapo ni Peter Msechu, Selemani Msindi (Afande Sele), Mwasiti Almas, Mwanahawa Abdul (Queen Darleen) na Clayton Revocatus (Baba Levo).
Wanamuziki hao ni miongoni mwa wanaounda kundi la Kigoma All Stars ambalo Zitto ametoa mchango mkubwa katika kuliendeleza.
Pia kulikuwapo wakereketwa wa Chadema ambao baadhi yao walimuuliza maswali. Mmoja wao alitaka Zitto aeleze ni kwa nini alivitaka vyama vya siasa vipeleke hesabu kukaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG).
Alihoji kuwa kwa kuwa kiongozi huyo alikuwa ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), pia Naibu Katibu Mkuu wa (Chadema), alikuwa na nafasi ya kuwaarifu wengine ndani ya chama chake kabla ya kufika hatua ya kutoa tamko kwa umma.
Akijibu swali hilo, Zitto alisema licha ya kuwa kufanya hivyo siyo utawala wa sheria na kutokutenda haki kwa vyama vingine, pia aliwahi kulizungumzia mara kadhaa ndani ya vikao vya chama.
“Nendeni mkawaulize kama mpaka leo mimi ni mmoja wa watu wanaotia saini utoaji wa fedha, nilijitoa baada ya kuona mambo hayaendi vizuri na nikahoji bila majibu,” alisema.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment