Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Saturday, November 23, 2013

Jengo la kibiashara laporomoka Latvia na kuua zaidi ya 30


Jitihada za uokozi zimeendelea katika jengo la kibiashara la Maxima baada ya kuporomoka,huko Latvia
Jitihada za uokozi zimeendelea katika jengo la kibiashara la Maxima baada ya kuporomoka,huko Latvia
au.news.yahoo.com

Na Martha Saranga Amini

Takribani watu 33 wamepoteza maisha huku 38 wakijeruhiwa na wengine zaidi hawajulikani walipo kufuatia kuporomoka kwa ghorofa la jengo la kibiashara mjini Riga nchini Latvian maafisa usalama wamearifu.

Jitihada za uokozi zimekuwa zikiendelea usiku kucha wakati huu ambapo jeshi la polisi likianzisha upelelezi kuchunguza tukio hilo.
Miongoni mwa waliopoteza maisha ni pamoja na waokoaji watatu ambao walikwama wakijaribu kuokoa watu waliokwama baada ya ghorofa nyingine zaidi kuporomoka.
Hata hivyo chanzo cha kuporomoka kwa jengo hilo hakijafahamika ingawa taarifa za awali zinabainisha kuwa kuna ujenzi ulikuwa unaendelea katika sehemu ya jengo hilo.
Taratibu za kukagua viwango vya ujenzi zinaendelea ili kubaini ikiwa kuna ukiukwaji wa usanifu majengo kwa Jengo hilo la kibishara ambalo lilifunguliwa mnamo mwaka 2011.
Waziri mkuu wa Latvian Valdis Dombrovskis ametembelea eneo la tukio na kusema jeshi la polisi tayari limeanza uchunguzi kuhusu tukio hilo.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment