Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, October 22, 2013

Mazungumzo ya amani Kampala yasitishwa.

Rais Joseph Kabila , wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, akiwa Addis Ababa, Ethiopia, kutia sini makubaliano ya amani ya kanda ya Maziwa Makuu. Sunday, Feb. 24, 2013.
Rais Joseph Kabila , wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, akiwa Addis Ababa, Ethiopia, kutia sini makubaliano ya amani ya kanda ya Maziwa Makuu. Sunday, Feb. 24, 2013.
Mazungumzo ya amani ambayo yamekuwa yakiendelea mjini Kampala
yakitafuta njia za kuleta na kudumisha amani mashariki mwa jamhuri ya
kidemokrasia ya Congo yamesimamishwa kwa muda. Hii ni  baada ya pande
mbili zinazoshiriki kwenye mazungumo haya kutofautiana Jumapili
kuhusu mmoja wa wajumbe wa M23- Roger Lumbala.

Mazungumzo hayo ambayo yalikuwa yakiendelea vizuri , Jumapili
ilitarajiwa kuwa ujumbe wa serikali ya Kinshasa na ujumbe wa M23
wangetia saini awamu ya kwanza ya makubaliano ambayo ilikuwa inahusika
na maswala ya kisiasa lakini hilo halikufanyika.

Roger Lumbala ni naibu kiongozi wa ujumbe wa M23 na alikuwa mbunge wa upinzani lakini mwaka uliopita akajiunga na kundi la waasi la M23.
Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo ni kubwa kuliko rais wake Joseph
Kabila na pia ni kubwa kuliko Roger Lumbala na kwa pamoja pande
zinazozozana zimekubaliana kuwa zinataka kuleta amani mashariki mwa
Congo kwa manufaa ya wakongomani wote.

Alipoulizwa kuhusu kuondoka meza ya mazungumzo ili majadiliano yaendelee Bw.Lumabala alisema "juu ya nini nijitoe wakati watu wanakufa watu hawapati chakula na mimi mni mcongo man ? kama wanataka amani tutaendelea kwa njia ya amani kama hawataki amani tufanya namna gani ?

Viongozi wa ujumbe wa serikali ya Congo umerejea mjini Kinshasa lakini
wajumbe wengine wangali mjini Kampala. Juhudi ya kupata maelezo ya serikali ya Kinshasa hazikufanikiwa.

Mazungumzo ya amani yalianza mjini Kampala mwezi wa Desemba mwaka jana.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment