Writen by
sadataley
5:02 AM
-
0
Comments
Jeshi la Nigeria limesema kuwa limewaua washukiwa 95 wa wapiganaji wa kundi la Boko Haram katika mashambulizi kaskazini mwa nchi hiyo,wakati wapiganaji hao walipopambana na vikosi vya usalama vya serikali katika eneo jirani.
Jeshi, ambalo linapambana kumaliza miaka minne ya machafuko ya kiislam nchini Nigeria, limesema kuwa limepeleka mabomu na vikosi vya askari wa nchi kavu kuharibu makambi ya waasi mjini Borno siku ya Alhamisi.
Msemaji wa jeshi Mohammed Dole amesema kuwa wanamgambo wapatao 74 waliuawa katika mashambulizi nje ya mji wa Maiduguri, ambako kundi hilo lilizaliwa zaidi ya mwongo mmoja uliopita.
Operesheni iliyosbabisha kuuawa kwa wapiganaji hao imekuja baada ya mauaji siku ya Jumatatu kwenye makambi ya Boko Haram katika sehemu nyingine ya mji wa Borno, ambako jeshi limesema liliwaua wapiganaji 37.
Katika tukio lingine la kuibuka kwa vurugu , washukiwa wa kundi la Boko Haram walishambulia kwa mawe mji wa Damaturu sambamba na uvamizi wa siku ya Alhamisi , na kuchoma majengo manne ya Polisi kwa mujibu wa afisa mmoja wa polisi.
No comments
Post a Comment