Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Saturday, July 20, 2013

Wanajeshi wa JWTZ waliokufa Sudan wawasili Tanzania.

Miili ya wanajeshi saba wa Tanzania waliokuwa katika kazi za kutekeleza ulinzi wa amani wa kimataifa katika mkoa wa Darfur nchini Sudan imewasili leo na ndege maalumu ya Umoja wa Mataifa.

Ujumbe wa umoja wa mataifa ukisaidia katika shughuli za uokozi wa majeruhi.
        Ujumbe wa umoja wa mataifa ukisaidia katika shughuli za uokozi wa majeruhi.
  Wanajeshi hao waliuwawa mwezi Julai, kufuatia shambulizi la ghafla wakiwa nchini Sudan.
Kaimu mkurugenzi wa habari wa JWTZ, Meja Joseph Masanja amesema miili hiyo imewasili  Jumamosi majira ya saa kumi kasorobo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu J. K. Nyerere na imehifadhiwa katika hospitali ya jeshi ya Lugalo hadi Julai 22 ambapo itaagwa rasmi.
Shughuli za kuagwa miili hiyo zitafanyika katika viwanja vya wizara ya ulinzi na jeshi la kujenga taifa vilivyoko Upanga jijini Dar es salaam.               

« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment