Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Monday, July 15, 2013

TANZANIA YATAKA SHERIA YA UMOJA WA MATAIFA KUBADILISHWA.

Tanzania inapendekeza kufanyiwa, marekebisho sheria ya kulinda amani, kuwezesha vikosi vya kulinda amani kujikinga na mashambulizi




Hii ni baada ya walinda amani saba wa Tanzania kuuawa na watu waliokuwa wamejihami eneo la Darfur mwishoni wa wiki.
Mauaji ya walinda amani 7 wa Tanzania nchini Sudan imewashangaza wengi sana nchini humo kulingana na naibu waziri mkuu kwani nchi hiyo ndio imeanza kushika kasi katika juhudi zake za amani kimataifa. .Wanajeshi wengi walijeruhiwa baadhi wako mahututi.
Maafisa hawakuwa na taarifa kamili kuhusu uvamizi wa Jumamosi ambapo wanajeshiu wengine 17 walijeruhiwa vibaya katika shambulizi baya zaidi kushuhudiwa dhidi ya vikosi vya kimataiofa nchini Sudan.
Shambulizi hilo lililofanywa na kikundi kikubwa cha watu waliokuwa wamejihami, ilihusisha mashambulizi makali ya mizinga na iliyolenga wanajeshi hao umbali wa kilomita 25 Magharibi mwa mji wa Khor Abeche.
Tanzania, ambayo pakubwa ni nchi salama na thabiti katika Kanda ya Afrika Mashariki, imeendelea kujitolea sana katika juhudi za amani duniani.
Mwaka jana ilikuwa nchi ya kwanza kujitolea kupeleka vikosi vyake Mashariki mwa Congo, chini ya kile ambacho kitakuwa kikosi cha walinda amani wa Umoja wa Mataifa wenye jukumu la kupambana vilivyo na makundi ya waasi huko.
Imewekwa na Happy Adam





« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment