Writen by
sadataley
7:30 PM
-
0
Comments
ANA UMRI WA MIAKA 50 TU NA TAYARI AMETEULIWA KUWA ASKOFU KATIKA KUSHREHEKEA SIKUKUU YA VIJANA DUNIANI

Baba Mtakatifu amemteua Padre Abdallah Elias Zaidan kuchukua nafasi ya Askofu Robert J. Shaheen aliyejiuzuru. Askofu Elias Zaidan ametangazwa rasmi leo hii na wajibu wake utaanza mara moja . Atakuwa ni Askofu wa Jimbo liitwalo Our Lady of Lebanon Eparchy.
Kabla ya uteuzi huo Askofu Zaidan alikuwa akitumika kama Kasisi wa kanisa Kuu huko Lebanon huko Lousiana.
Askofu Zaidan alizaliwa huko Kosaybé, Lebanon mwezi March 10, 1963 katika maisha yake ya utumishi amekuwa mmoja wa wafuasi wa shirka la Walebanoni na ametumika katika tume mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufanya kazi kama mtawala katika shule na kufanya utume wa Kichungaji katika Parokia mbalimbali.
Askofu Zaidan licha ya kuzungumza lugha ya Kiingereza pia anauwezo wa kuzungumzaa Kiarabu,Kifaransa, Kiitalia, Kihispania na Kisiria.
No comments
Post a Comment