Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, July 16, 2013

HALI YA MISRI SI SHWARI VURUGU ZAPAMBA MOTO.

Mamia ya wafuasi wa kiongozi aliyepinduliwa Misri Mohamed Morsi wamepambana na vikosi vya usalama katikati mwa mji wa Cairo na kuwafyatulia waandamanaji hao gesi ya kutoa machozi.

 Mamia ya wafuasi wa kiongozi aliyepinduliwa Misri Mohamed Morsi wamepambana na vikosi vya  usalama katikati mwa mji wa Cairo.

Mapigano hayo yanajiri muda mfupi baada ya mjumbe mkuu wa Marekani William Burns kutoa wito kwa vikosi vya usalama kujizuia kwa kiwango kikubwa katika kukabiliana na maandamano hayo
Makabiliano yalifanyika baada ya naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani anayezuru Misri, kuwataka maafisa wa usalama kuhakikisha kuwa wanajitahidi kutuliza ghasia wakati wakijizuia kufanya mauaji yoyote.
Burns alikutana na maafisa wa serikali inayoungwa mkono na majeshi.
Lakini chama cha Muslim Brotherhood kimesema haikina nia ya kukutana na waziri huyo.
Akizungumza baada ya kukutana na viongozi wa serikali mpya inayoungwa mkono na jeshi nchini, mjumbe huyo, William Burns, amesema Misri imepewa nafasi ya pili kufuatia kupinduliwa na jeshi Mohammed Morsi.
Alikutana na serikali inayoungwa mkono na jeshi nchini lakini Muslim Brotherhood, inasema haina mpango wa kukutana naye. Naibu rais wa tawi la kisiasa la chama cha Morsi, Muslim Brotherhood,Essam el-Erian
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment