Writen by
sadataley
8:24 AM
-
0
Comments
Rais John Pombe Magufuli wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemsifu mtangulizi wake Rais msaatafu Jakaya Mrisho Kikwete na kusema kwamba, kama sio Kikwete leo asingekuwa Rais wa nchi hiyo.
Rais Magufuli amesema kwa kazi kubwa ambayo imefanywa na Rais mstaafu Jakaya Kikwete kwenye uongozi wake kuna mambo makubwa ya maendeleo katika nchi hiyo huku akitanguliza uzalendo mkubwa ambapo Watanzania wanamkumbuka na wataendelea kukumbuka watake wasitake.
Rais Magufuli amesema hayyo katika uzinduzi wa Taasisi Isiyo ya Kiserikali ya Jakaya Mrisho Kikwete(JMKF) na kubainisha kwamba, ipo mifano mingi hai ya mambo ambayo ameyafanya Rais mstaafu Kikwete kwenye Serikali ya Awamu ya nne na baadhi ya miradi hiyo lipo la ujenzi wa bomba la gesi kutoka mkoani Mtwara hadi Dar es Salaam, ujenzi wa miundombinu ya barabara nchi nzima, ujenzi wa miradi ya maji , umeme na kuimarisha sekta muhimu za afya, kilimo na vijana.
Rais Magufuli amesema: "Uzalendo wa mzee Kikwete kwa nchi yake umemfanya hata baada ya kustaafu kuamua kuanzisha taasisi ambayo amiezindua rasmi na vipaumbele vya taasisi hiyo havina tofauti na vile ambavyo anavitekeleza kwenye Serikali yake, hivyo ameahidi kumpa ushirikiana mkubwa kufanikisha malengo hayo na kuomba wadau wengine wakiwamo mabalozi nao kuunga mkono kazi za taasisi hiyo."
Kwa upande wake Rais Mstaafu Kikwete amesema kuwa anamshukuru Rais Magufuli kwa kukubali kuzindua taasisi hiyo na kuipa heshima ya hali ya juu na kutumia nafasi hiyo kuahidi kuwa lengo la kuanzishwa kwa taasisi hiyo ni kufanya kazi katika maeneo ambayo wameamua kuanza nayo zaidi kama sehemu ya kutoa mchango wao katika kushirikiana na Serikali kutekeleza majukumu yake.
Parstoday
No comments
Post a Comment