UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

Saturday, April 7, 2018

Marehemu ajali ya City Bus waagwa leo

Mamia ya wakazi wa wilaya ya Igunga na maeneo jirani wamejitokeza katika hospitali ya wilaya ya Igunga kuaga miili12 ya marehemu waliofariki katika ajali ya basi iliyotokea usiku wa April 4 katika kijiji cha makomelo ambayo ilihusisha basi la kampuni ya City boy, lililokuwa likitoka karagwe mkoani Kagera kuelekea Dar es salaam na loli aina ya Mitsubishi fuso.

Ni huzuni na simanzi vimetanda katika eneo la hospital ya wilaya ya Igunga wakati wa kuaga miili ya marehemu waliofariki katika ajali ya basi.

Akitoa salam za Raisi wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amewapa pole wote walioondokewa na wapendwa wao huku akisisitiza kuwa serikali haitafumbia macho yeyote aliyehusika kufanya uzembe na kusababisha ajali hii.

Aidha idadi ya waliofariki imeongezeka na kufikia watu 13 baada ya mmoja aliyekuwa akipatiwa matibabu katika hospital ya rufaa bugando kufariki dunia ambapo hadi sasa miili iliyotambuliwa ni tisa na miili mitatu bado haijatambuliwa.

Jamii ikaaswa kuendelea kutenda mema maana hakuna aijue siku ya kifo

Bwana alitoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment