Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, March 7, 2018

Yanga SC wawaomba Jezi Waarabu


KATIKA hali ya kush­angaza juzi Jumatatu, baadhi ya makoman­doo wa Yanga na mashabiki waliamua kuvamia mazoezi ya Al Masry na kuomba jezi ili waweze kuishangilia timu hiyo katika mchezo wa dhidi ya Simba, huku wakisikika wak­isema ‘Simba 1 Al Masry 3’.

Katika mchezo huo ambao unapigwa leo Jumatano saa 12 jioni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, makomandoo hao hawakusita kuonyesha ushabiki wao kwa timu hiyo wakati wakifan­ya mazoezi juzi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam huku wakilitaja jina la mshambuliaji wa timu hiyo, Aristide Bance raia wa Burkinafaso.

Makomandoo hao walifika uwanjani hapo kuangalia maz­oezi ya wapinzani wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Township Rollers kabla ya mchezo wao uliopigwa jana kwenye Uwanja wa huo am­bapo timu hiyo ilipomaliza maz­oezi na kuwapisha Al Masry, wao walikomaa na kuwafuata viongozi ili wawape jezi watakazovaa leo na kuwashangilia.

Championi ambalo lilikuwepo uwanjani hapo liliwashuhudia makomandoo hao wakijadiliana kuwaomba jezi viongozi hao kabla ya kuwafuata lakini hawakuweza kufanikiwa kwa kuwa wajibiwa kuwa:” Mtatusamehe, hatujabeba jezi za kutosha.”

“Lazima Simba itafungwa mabao 3-1, nawahakikishia na wale msiwe na hofu hata kidogo,” alisema komandoo mmoja wa Yanga wakati anahojiwa na kituo kwa One Sport cha Misri.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment