Writen by
sadataley
9:15 AM
-
0
Comments
Wahajiri wa Kiafrika wamefanya maandamano katika mji wa Florence nchini Italia wakipiga nara za kulaani ubaguzi wa rangi na kupinga mauaji ya mhajiri wa Kiafrika yaliyofanywa na raia wa Italia.
Polisi ya Italia inasema muuzaji bidhaa za barabarani kutoka Senegal aliuawa mapema Jumatatu iliyopita kwa kupigwa risasi sita na Mtaliano aliyejulikana kwa jina la Roberto Pirrone.
Mauaji na maandamano hayo yamefanyika siku moja tu baada ya uchaguzi mkuu wa Italia ambao umeshuhudia wagombea wengi wakiwataja wahajiri wa kigeni kuwa ni wahalifu na wametoa wito wa kufukuzwa wahamiaji nchini humo.
Mjumbe mmoja wa Wasenegali wanaoishi Italia amesema kuwa, anga iliyotawala kinyang'anyiro cha uchaguzi mkuu na mafanikio ya muungano wa wapinzani wa wahajiri katika uchaguzi huo ndivyo vilivyochochea mauaji hayo. Ameongeza kuwa, Italia sasa inaelekea kuwa nchi ambayo watu weusi wanauawa kirahisi katika mitaa ya miji yake.
Mwezi ilopita pia mfuasi mmoja wa chama kinachowapiga vita wahajiri nchini Italia aliwafyatulia risasi wahajiri wa Kiafrika katika mji mmoja wa nchi hiyo na kujeruhi 6 miongoni mwao.
Parstoday
No comments
Post a Comment